Monday, March 12, 2012

........SHOO NYINGI FILAMU HAKUNAGA KWA MUDA..........

MSANII wa filamu ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye muziki, Shilole (mkali wa mauno), amedai kuwa endapo kama atapata kazi nyingi za kufanya shoo anaweza kuachana na filamu kwa muda kwani tayari mashabiki wengi wameanza kujitokeza katika shoo  zake.

Hayo aliyasema wakati akizungumza na mwandishi wetu, juu ya maisha yake ya sanaa pamoja na mpangilio wake wa muda kwani kwa sasa anaonekana zaidi kwenye matamasha ya muziki kuliko filamu.

Alisema yupo mjini kwa lengo la kutafuta pesa hivyo endapo atakuwa bize na shoo za muziki anaweza kusimama kwa muda kufanya filamu kwani kila kitu kinaenda kwa ratiba.

“Endapo nitakuwa bize sana na muziki naweza kusisima kwa muda kucheza filamu, kwa sababu kila kitu kinaenda kwa ratiba lakini hata hivyo siyo kwamba kwa sasa sifanyi filamu kazi ipo palepale,” aliema.

Aliongeza kuwa fani ya muziki imeweza kumtoa katika maisha fulani na kumpeleka hatua nyingine ambayo anamshukuru mungu kwani anaamini baada ya miaka kadhaa mbele anatakuwa mbali zaidi.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms