Monday, March 19, 2012

...........RUSSEL ANASAKWA NA POLISI.........

MCHEKESHAJI Russell Brand anatafutwa na polisi kwa kosa la kumnyang'anya na kuitupa simu ya mwandishi wa habari aina ya iPhone.

Tukio hilo lilitokea katika mitaa ya jiji la New Orleans, ambako mchekeshaji huyo alikuwa akikatiza na mwandishi wa habari ghafla alianza kumpiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Russell baada ya tukio hilo aliandika katika mtandao wa twitter kuwa alifanya tukio hilo kumuenzi mbunifu wa simu hizo, Steve Jobs aliyefariki mwaka jana.

"Tangu Steve Jobs afariki huwa naumia sana roho ninapomuona mtu anaitumia vibaya simu aina ya iPhone, ndiyo maana nikaamua kuitupa ile simu kwa kuwa yule mwandishi alikuwa akiitumia vibaya," aliandika Russell.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms