Thursday, March 8, 2012

........RAMSEY, DANIEL LLORD KUJA KIUPYA ZAIDI......

WIKI chache zilizopita kulikuwa na habari kwamba nyota wa Nollywood, Ramsey Noah na Daniel Lloyd, waliumia vibaya wakati walipokuwa wakitengeneza filamu, sasa Daniel ameibuka na kuelezea mkasa mzima.

Mwigizaji huyo alisema kuwa walikuwa wakijaribu kupigana wakati walipokuwa wakitengeneza filamu, kwa bahati mbaya wakafyatuliana risasi.

Noah aliumia kichwani na mimi nilijeruhiwa mkononi, lilikuwa ni jambo baya sana, alisema.
Lakini sasa tunaendelea vizuri, baada ya muda mfupi tutarudi katika uigizaji kwa mara nyingine.
Aliongeza kuwa baadaye wataanda filamu ambayo itawashirikisha Tonto Dike na Rukky Sandra.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms