Tuesday, March 13, 2012

........OGE OKOYE ATAMANI KUZAA WATOTO 10.....

OGE Okoye anasema atazaa hata watoto kumi kama Mungu amempangia hivyo kwani aliokwisha zaa hadi sasa (wawili), hawampi presha yoyote kwenye kazi zake za kila siku.

Nina mtoto wa kike na wa kiume. Ninajivunia sana kuwa nao na namshukuru Mungu kwamba mimi ni mwanamke mkamilifu mpaka sasa. Raha ya mama ni kuwa na mtoto wa kike na wa kiume, tulianza na mvulana na sasa tuna msichana,alisema.

Wala hawanipi presha, nilipojifungua mtoto wa kwanza nilipata msaada kwa kila rafiki na ndugu, wala sikutaka mambo ya filamu yaathiri uwepo wangu kama mama wa familia, kila kitu nilikuwa nafanya kwa wakati wake na mpaka sasa nafanya hivyo hivyo.

Mtoto wangu wa kiume tayari ameanza shule na huyu wa kike ni mkubwa anaendelea na mambo yake kama kawaida, kuwa nao hakuathiri kiwango changu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms