Sunday, March 4, 2012

......NIMEHAMIA MASHUJAA??? NANI KASEMA??? UZUSHI BWANA.........

Mwanamuziki amekanusha habari kwamba yuko mbioni kuihama bendi yake ya Ngwasuma.
Patchou Mwamba ameongea asubuhi hii na Spoti Starehe na kukanusha habari hizo zilizoenea kwa mashabiki kuwa ameahidiwa kupewa gari na Million 20 ili ahamie bendi ya Mashujaa.
Bendi ya Mashujaa ambayo kwa sasa inajizolea umaarufu hasa baada ya kumtwaa muimbaji na mtunzi nguli wa Twanga Pepeta Chars Baba “Tores” ambaye kwa kiasi kikubwa ameimarisha kikosi cha Mashujaa Band.
Patchou eambaye kwa sasa mejizolea umaarufu mkubwa wa kuigiza kwenye thasmia ya Bongo Movie amesema kuwa si kweli habari hizo ni uongo tu “…. Uncle si kweli habari hizo si za kweli na ni uzushi … akapumua kidogo akacheka kisha akendelea …. mi bado nipo FM na nitaendelea kuwepo na kwa sasa tunarekodi nyimbo mpya kwa ajili ya albamu nyingine ambayo itajulikana kama Chuki ya Nini…” Aliongeza Patchou ambaye Spoti na Starehe ilimkurupua Usingizini.
Alikadhalika Patchou amekanusha uvumi mwingine kuwa Presidaa Nyoshi ametimkia Uingereza na kuwa amejiunga na Bendi ya Wacongo ambayo wanaishi huko Uingereza. “…Nyoshi amekwenda mapumzikoni na atarejea hizo zote ni uzushi mtupu”.
Akiongea jana na kukaririwa na Spoti na Starehe shabiki mkubwa wa Bongo Dance ambaye hakutaja jina lake niliandike bloguni amesema kuwa habari za PAtchou Kuondoka ni za ukweli kabisa na Mashujaa wamemuahidi Verosa na Milioni Ishirini na atalipiwa nyumba ili aondoke FM…. “Patchou ananondoka FM na ameahidiwa Milioni ishirini pamoja na Toyota Verosa na Mama Sakina atamchukua kweli…” Kilisema chanzo hicho kwa kujiamini.
Mashujaa Band inayomilikiwa na Mama Sakina inasemekana iko kwenye mikakati ya kujiimarisha kwa sasa na inampango wa kuchukua wanamuziki kadhaa na mmoja wa waliokuwa wakitajwa ni mwanamuziki Patchou Mwamba.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms