Friday, March 9, 2012

.........NIKO JUU KULIKO MFANO.........

MSANII wa filamu bongo , Salma Jabu ‘Nisha’, ameibuka na kusema kuwa,  yupo juu na kwasasa yuko  mbioni kuachia kazi yake mpya inakwenda kwa jina la ‘Macho Yangu’ ambayo itakuwa na wasanii wengine kibao.

Nisha alisema kuwa ndani ya filamu hiyo yenye amecheza kama bubu, ambaye hawezi kuzungumza.

Wengine ni Flora Mvungi ambaye amecheza kama mtoto wa kishua ambaye kwao kuna fedha chafu, pia Shilole ambaye amecheza kama taahira, Cojack amecheza kama jambazi, pia kuna mzee Hashimu Kambi ambaye amecheza kama baba wa Flora Mvungi.

Hata hivyo aliongeza kuwa hiyo ni filamu yake mwenyewe kwani mwaka huu amejiwekea mikakati ya kufanya kazi zake mbali na zile anazoshirikishwa na wasanii wengine kama, Ray, P.H.D, Jackline Wolper na wengine.

“Mwaka huu nimejiwekea mikakati ya kutoa filamu zangu mwenyewe hivyo naamini mambo yatakuwa mazuri kwa sababu tayari naanza na hiyo ambayo itakuwa moto wa kuotea mbali,” alisema.

Hata hivyo msanii huyo aliwaomba mashabiki wake kuisubili kazi hiyo kwani ipo kwenye hatua za mwisho.

5 comments:

wajanjaclub said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

Huyu dada yuko juu ile mbaya. Ana TATOO bomba sijawahi kuona. namzimikia ile mbaya

Anonymous said...

Huyu dada yuko juu ile mbaya. Ana TATOO bomba sijawahi kuona. namzimikia ile mbaya

Anonymous said...

Huyu dada yuko juu ile mbaya. Ana TATOO bomba sijawahi kuona. namzimikia ile mbaya

Anonymous said...

Huyu dada yuko juu ile mbaya. Ana TATOO bomba sijawahi kuona. namzimikia ile mbaya

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms