Wednesday, March 21, 2012

..........NIKO FITI KWENYE GAME ILE MBAYA.....


MWANADADA anayetesa katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper amesema mara nyingi huzingatia maelezo na kushika muongozo, jambo linalomjenga na kuwa nyota na kuwafunika wasanii wenzake wa kike.

Hivi karibuni, mrembo huyo alionekana katika filamu ya Dereva Taxi ambamo aliigiza kama msichana mtukutu.

Nimejitoa kuigiza katika kiwango cha juu, kila siku nahitaji kuwa bora zaidi ya kazi iliyopita kwa sababu hii ni kazi yangu na naipenda, baada ya kutoka filamu ya Dereva Taxi, baadhi ya watazamaji wanajua kuwa mimi ni binti mtukutu na mkorofi, kumbe ni uhusika tu wala sipo hivyo.

Mimi ni mtulivu kabisa, ni muongozo ulifanya nifanye hiyvo, anasema.

Jack ni mwigizaji anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahiliwood kutokana na mavazi yake na kuigiza katika kiwango cha juu. Filamu alizoshiriki msanii huyo ni Last Minutes, Surprise, Secretary, All About Love, na Dereva Taxi inayokimbiza mtaani kwa sasa.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms