Monday, March 19, 2012

..........NICK MINAJ AWEKA WAZI KUHUSU JAY Z.........

RAPA wa kike Nick Minaj, amesema anatamani mafanikio aliyonayo Sean Carter, maarufu kama Jay Z, na kuahidi kuwa anafanya kila liwezekanalo ili aweze kuivunja rekodi yake.

Minaj anasema, malengo yake kwa sasa ni kufikia mafanikio ya rapa huyo mwenye utajiri unaokadiriwa kuwa Dola 450 milioni.

"Niliwahi kukutana na Jay Z ambaye alinipongeza kwa mafanikio yangu katika muziki, lakini moyoni nilikuwa najisemea; 'lazima nikupiku Jay Z'," anasema Minaj.

Nick anasema kimuziki amejitahidi, lakini kitakachomfanya amfikie Jay Z ni kujiingiza katika biashara na huo ndio mpango wake wa sasa.

"Baada ya kutoa albamu nyingine, nitapumzika kutengeneza muziki kwa muda na kujikita katika biashara, ambazo bado nazifanyia utafiti iwapo zitanilipa na kunifanya bilionea kama Jay Z," alisema Minaj.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms