Tuesday, March 20, 2012

.......NGOMA YANGU YA MAZOEA KUJA KUWASHIKA.....


BAADA ya kumtoa Bi Cheka, msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka TMK, Mh Temba, amesema kuwa anatarajia kutoa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mazoea’, ambayo itatoka sambamba na video yake.

Msanii huyo ambaye amekuwa mstali wa mbele kuwatoa nyota chipukizi, alisema kuwa wimbo huo ndiyo utakaokuwa wa kwanza kwa upande wake na anaamini utakuwa moto wa kuotea mbali.

Alisema kuwa ngoma hiyo haitakuwa kuwa na mfano kwani muziki wake anafanya tofauti na wasanii wengine hivyo mashabiki wake wake mkao wa kula kuweza kuona ujio wake mpya.

“Hiyo ndo ngoma yangu mpya ambayo ambayo itakuwa sokoni April mwaka huu hivyo nawaomba mashabiki wangu wawe na uvumilivu kwani sitaki kufanya kitu kwa haraka baada nije kuharibu,” alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms