Thursday, March 8, 2012

..........NARUDI KUWAFUNIKA.........

MWIGIZAJI nyota na mkongwe katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Salama H. Salmin Sandra, amefunguka kwa kusema anarudi katika tasnia hiyo kwa nguvu zote na lengo ni kuwapoteza wasanii wa kike wanaotamba kwa sasa.

Anasema pamoja na kuwa kimya kwa muda mrefu, alikuwa akisoma mchezo unavyokwenda na kubaini kuwa yeye bado yupo juu na hana mpinzania katika fani hiyo.

Kwa sasa katika tasnia ya filamu kuna ushindani mkubwa hasa kwa akina dada. Kila msanii anaonyesha uwezo katika kuigiza, alisema.
Lakini mara zote ninapoangalia kazi za wapinzani wangu, huwa nayaona mapungufu mengi na jambo hilo ndiyo limenifanya niamue kurudi.

Narudi kuwafunika na kuwapoteza kabisa na hilo utaliona katika filamu ya Toba.

Sandra amesema kuwa kwa sasa yupo huru baada ya mtoto wake wa pili, Arqaam, kukua na kuweza kukaa na Yaya.

Katika filamu ya Toba inayorekodiwa sasa, wasanii wengine wanaoshiriki ni pamoja na Chiki Mchoma, Suleiman Barafu na Issa Mussa Cloud 112 anayeshiriki kama mume wa Sandra.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms