Thursday, March 29, 2012

..........MSINICHAFULIE UCHUMBA WANGU JAMANI......

MWIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Rose Ndauka Aisha, ameibuka na kusema kuwa watu wanajaribu kumharibia na kumtangazia tabia ambayo si yake, jambo ambalo linamchafua mbele ya jamii.

Inasemekana tangu mrembo huyo mwenye jina katika tasnia ya filamu aanze kuishi kama mke amekumbwa na kashfa nyingi huku akiambiwa kuwa sasa anatumia kilevi.

Hali hiyo imewafanya baadhi ya wanajamii kuhisi huenda mwanadada huyo kakumbwa na msongo wa mawazo.

Mwanaspoti lilimtafuta Rose na kuzungumza naye kuhusu shutuma zinazomkabili kama chanzo ni uhusiano huo mpya au la.

Ni kweli, hata mimi kuna baadhi ya maneno nayasikia kuhusu uhusiano wetu na mwezangu, lakini si ya kweli, na ikumbukwe kuwa sisi bado ni wapenzi, kwani hatujafunga ndoa.
"Kwa hiyo hata mtu akiniuliza maisha ya ndoa siwezi kumjibu kwa sababu bado sijaishi, kwa sasa tupo katika uchumba na maisha yetu yako poa, anasema Rose.
Pia amesema kuwa uhusiano wake na mpenzi wake si tatizo kwani hazuiwi kufanya lolote linalohusu filamu, lakini anapopata kazi ni vema kumjulisha mwenzi wake kwa sababu hana kipingamizi kwani huko ndiko alikomuona.

Anasema yeye ana uhuru wa kufanya kazi wakati wowote ilimradi iwe na maslahi kwake, huku akiongeza kuwa uhusiano wake na mpenzi wake uko shwari.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms