Sunday, March 4, 2012

...........MIMI NI MKALI KULIKO WAO......LOL, HAHAHAHA..........


MSANII wa filamu bongo Chiristine John ‘Sintah’, amedai kuwa kati ya Kajala na Jackline Wolper, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kumfikia katika kiwango chake cha uigizaji.

Msanii huyo alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hizi, ambapo alisema nyota hao hawana ubunifu katika zao ndiyo maana anawahesabia kama wanafunzi.

Alisema endapo watapata nafasi ya kucheza filamu moja anaweza kuonesha anachokisema kwani hawana uwezo wa kumtisha katika kiwango chake.

Alisema kuwa hao wote wanacheza filamu lakini kitu kikubwa wanachokosea ni kwamba wanakosa ubunifu katika filamu zao kitu ambacho kila siku wataonekana bado wanako chini.

“Msanii lazima uwe mbunifu hivyo endapo ukikosa kitu hicho basi huwazi kujihesabia kama ni msanii,” alidai Sintah.

Hata hivyo aliongeza kwa katika kuonesha kwamba ana ubunifu katika filamu zake sasa yupo katika maandalizi ya kazi ya filamu zake mbili ambazo zitakuwa katika kiwango cha kimataifa.

Filamu hizo ni ‘Sitaki Demu’ na ‘Return of Jlo’, ambazo hazitakuwa na nyota wale ambao wanaonekana kila siku kwenye filamu ambazo hazina ubora.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms