Friday, March 30, 2012

........MILLEN MAGESE AWAPA ULAJI WANAMITINDO WA TANZANIA.....

WABUNIFU watatu wa Tanzania watashiriki maonyesho ya mitindo ya Wiki ya Mitindo Afrika Kusini kupitia Kampuni ya Millen Magese Group Limited.

Wabunifu hao watapanda jukwaani Aprili Mosi katika onyesho linalobeba jina la Tanzania International Fashion Expos (TIFEX) by Millen Magese introducing Eskado Bird, Jamila Vera Swai and Evelyne Rugemalira.

Wabunifu hao ni Doreen Estazia Noni anayetumia Lebo ya eskado bird, Jamila Vera Swai na Evelyne Rugemalira.

Millen alipata fursa ya kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa wabunifu katika fani hiyo na kushawishika kuwachukua kushiriki maonyesho hayo.

Alisema kuwa amevutiwa na jinsi walivyokuwa wabunifu na hivyo kuhamasika kuwapa nafasi hiyo ya kujitangaza kimataifa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kupitia mradi huu ambao pia dhumuni lake ni kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa.

Alisema mpango huu pia una lengo la kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo dunia nzima kama New York fashion week, London Fashion Week, Lagos Fashion week na Milan Fashion week.

"Hii ni nafasi ya wabunifu wa Tanzania kujitangaza kimataifa," alisema Magese na kuongeza kuwa yote yanawezekana kutokana na uzoefu wake wa miaka nane katika fani ya mitindo na mahusiano mazuri kati yake wadau wa mitindo.

Mbali ya wabunifu hao, Millen pia amewapa nafasi wanamitindo watatu, Anastazia Gura (21) na mapacha, Victoria Casmir (20) na Victor Casmir kuonyesha mitindo katika maonyesho hayo ya Afrika Kusini.

Wanamitindo hao wamepata nafasi hiyo baada ya kuwashinda wengine 486 waliofika katika usaili uliofanyika kwenye hotel ya Serena chini ya majaji, Mustapha Hassanali, Ritha Poulsen na mwanamitindo maarufu Aminat Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12.

Mbali ya wanamitindo hao Millen pia ameingia mkataba wa kufanya kazi na mwanamitindo wa kiume, Benard Chizi ambaye pia alishinda katika usaili huo na pia ataungana na wenzake kwenda Afrika Kusini.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms