Monday, March 5, 2012

........MERYL STREEP AUSHANGAZA ULIMWENGU..........


MWIGIZAJI, Meryl Streep, ameweka historia kwa kutwaa tuzo nyingine ya Oscar, baada ya kuibuka Mwigizaji Bora wa mwaka huu.
Ushindi huo wa juzi unamfanya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 63, kufikisha tuzo tatu za Oscar.

Hakuna mwigizaji aliyewahi kushinda tuzo nyingi kumshinda yeye katika historia ya tuzo hizo ambazo mwaka huu zimefanyika kwa mara ya 84.

Si tu amekuwa mtu wa kwanza kushinda tuzo nyingi za Oscar, mwigizaji huyo ndiye mtu pekee aliyewahi kupendekezwa mara nyingi kuwania tuzo hizo. Amewahi kupendekezwa mara 17.

Amewahi kushinda tuzo hizo mwaka 1979 alipoigiza katika Kramer vs. Kramer, akashinda tena mwaka 1982 alipoigiza katika Sophies Choice na mwaka huu ameshinda baada ya kuigiza katika Iron Lady.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms