Friday, March 9, 2012

........MCHEZAJI WA BARCELONA 'CESC' AKIRI KUFANYA MABADILIKO........

Mchezaji wa Barcelona Cesc Fabregas amekubali kwamba Mwanzoni alipoondoka Arsenal na kujiunga na Barcelona, ilikuwa vigumu kubaki katika nafasi yake uwanjani, alikuwa akitoka na kushambulia mara nyingi kitu ambacho anaamini alikifanya kwenye mechi nne au tatu.
Amesema alikuwa akiwaona Alves na Alexis wanakimbia kwenda kushambulia nae anawafata lakini siku hizi amefanya maamuzi ya kubaki nyuma, amesema Labda watu wanaweza wasiamini hili lakini kwake wazo kubwa zaidi ni kufikiria timu na sio yeye binafsi, na ilijidhihirisha kwa mechi na Bayer Leverkusen, hilo ni moja kati ya mabadiliko makubwa aliyoyafanya toka amerudi Barcelona.
Jana Barcelona waliichapa Bayern Leverkusen 7 -1 huku Lionel Messi akiondoka na magoli yake matano.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms