Thursday, March 15, 2012

......MAISHA YA WAIGIZAJI NI DUNI..........

MASHAKA ambaye ni mwigizaji mkongwe katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, amesema kuwa kuigiza vizuri siyo kigezo cha kuwa na maisha bora, akiamini ingekuwa hivyo basi wao wangekuwa matajiri wakubwa.

Kuigiza vizuri siyo kufanikiwa kimaendeleo. Hapa Tanzania inaweza kuwa ni bahati tu au kuna kitu kingine mtu anakifanya ndiyo kinamwingiza fedha, alisema.

Pia akizungumzia sanaa, anasema kuna wasanii wengi aliowafundisha na kati ya hao ni wawili tu wanaoweza kusema ukweli kuwa Mashaka ametuonyesha njia katika sanaa, nao ni Cloud na Riyama Ali.

Mashaka pia anamtaja mchekeshaji Kingwendu akisema bila yeye inawezekana kabisa asingeingia katika tasnia ya filamu na maigizo.

Lakini si rahisi kwa mtu kusema mbele za watu kuwa bila fulani nisingekuwa hapa, alisema.

Mashaka kwa sasa yupo katika mikakati ya kuhakikisha kundi la Kaole Sanaa linarudi katika hadhi yake kama awali.

Kaole ni sawa na chuo kwani ukifuatilia kwa karibu utagundua kuwa asilimia kuwa ya wasanii wakubwa wanaofanya vizuri, wengi wamepitia Kaole, alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms