Monday, March 19, 2012

.........KIM KARDASHIAN ABWATUKA......

STAA Kim Kardashian amesema anamfungulia mashtaka daktari mmoja nchini Mexico, kwa kutumia picha yake kuitangaza kliniki yake inayojihusisha na urekebishaji wa maumbile ya wanawake kama vile pua, midomo, makalio na matiti.

Kim amesema amefikia hatua hiyo kwa kuwa siyo tu kutumia picha yake bila idhini yake ni makosa, bali pia ni kumdhalilisha kwani watu watadhani hata yeye huwa anayachonga mwili wake.

Tangazo hilo linamuonyesha Kim akiwa amevaliwa nguo za kuogelea, huku likiambatana na maandishi yasemayo 'iwapo unataka kuchongwa kwa ustadi kama Kim, muone daktari huyo'.

Jarida la TMZ lilipomtafuta daktari huyo na kumuuliza iwapo aliwasiliana na Kim juu ya tangazo hilo, alisema hamfahamu mtu huyo na aliitumia picha hiyo baada ya kuiona mtandaoni.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms