Thursday, March 8, 2012

......KIBOKO WA LILIAN INTERNET HUYU HAPA..........

Hivi majuzi ilitangazwa mcheza sho wa Twanga Pepeta Lilian Internent ametimkia Mashujaa Band, mwenyewe akikaririwa akisema maslahi ndio yamempeleka huko.
Habari za mashabiki zinasema kuwa Lilian ambaye alipata umaarufu sana kutokana na uchezaji wake ambao uliwavutia mashabiki amekimbizwa na mwanadada huyu mahiri anayejulikana kama Fasha Joshua.
Mwanadada Fasha anakubalika na mashabiki na kwa sasa anapeleka vilivyo ndani ya ngome ya Twanga. MAshujaa pamoja na Lilian Internet pia wamemchukua aliyekuwa mpiga solo wa Twanga Ally Akida.
Lilian na Ally Akida kwa pamoja wamsaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Mashujaa Musica na watatambulishwa Jumatano hii ndani ya ukumbi wa Nyumbani Lounge.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms