skip to main |
skip to sidebar
8:08 AM
wajanjaclub
Ishu ya mastaa wawili wa kike Bongo, Judith Wambura ‘Jide’ na Jacqueline Patric ‘Jack’ kujipanga namna mazishi yao wanavyotaka yawe watakapoaga dunia, imezua kizaazaa ikielezwa kuwa wana pepo mbaya wa kifo.
Mbali na watu wa kawaida kwenye jamii kulaani kitendo hicho, mtumishi wa Mungu aliyejitambulisha kwa jina la Faustine Mwijage Kamugisha wa jijini Dar aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa amesikitishwa na wanadada hao akidai kuwa ni kinyume na matakwa ya Mungu hivyo wanaongozwa na pepo wa kishetani.
“Huku ni kumkufuru Mungu, wameingiwa na pepo wa shetani, kujipangia mazishi maana yake unajiwekea mipango ya kitu ambacho huna uwezo nacho, huko ni kutenda dhambi bila kujua.
“Kifo ni lazima kwa mwanadamu, lakini huwezi kujipangia kifo wala mazishi yako hata siku moja,” alisema mchungaji huyo na kuongeza:
“Wasome Yeremia 17:9, maandiko yanasema, Moyo huwa mdanganyifu. Hapo ina maana hao wameshadanganywa na shetani na ni vigumu wao kugundua kwani shetani naye ana nguvu zake hivyo wanahitaji maombi.”
Hivi karibuni Jide ambaye ni mwanamuziki mkubwa Bongo na Jack (modo maarufu), waliweka bayana namna na ratiba ya mazishi yao pindi watakapokufa ambapo gazeti hili limesheheni maoni ya watu mbalimbali waliokosoa na kulaani ishu hiyo.
0 comments:
Post a Comment