Tuesday, March 6, 2012

.......JENNIFER KUPANDA KIZIMBANI.......

JENNIFER Hudson atakuwa mmoja kati ya watu watakaotoa ushahidi katika kesi ya mauaji ya mama yake mzazi, kaka yake na mpwa wake waliouawa mwaka 2008.

Jina la mwimbaji huyo limewekwa kwenye orodha ya watu wanaohitajika kutoa ushahidi katika kesi hiyo itakayoanza kusikilizwa Aprili 9.

Katika kesi hiyo mume wa dada yake, William Balfour, anashtakiwa kwa mauaji hayo yaliyotokea, Oktoba 2008 huko Chicago.

Huson anakuwa shahidi wa kwanza baada ya kumtaja mwanamume huyo katika maelezo yake ya awali, huku akisema kuwa aliwahi kumuonya dada yake asikubali kuolewa na mwanamume huyo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms