Monday, March 5, 2012

........HARUSI YA BRITNEY SPEARS HAKUNAGA........


NDOA ya mwanamuziki, Britney Spears na mchumba wake, Jason Trawick, imesogezwa mbele baada ya mawakili wa mwanamuziki huyo kumshauri afanye hivyo.

Mawakili wake wamemshauri aachane na masuala ya ndoa, mpaka pale kesi yake dhidi ya meneja wake wa zamani, Sam Lutfi, itakapofikia tamati.

Mwanamuziki huyo amefunguliwa mashtaka na meneja huyo ambaye anadai kuwa hakuridhika baada ya kufukuzwa kazi.

Mahakama imeamua kuwa mali na biashara zote za Spears, zisimamiwe na baba yake mzazi, Jamie Spears, mpaka kesi itakapomalizika.

Kwa maana hiyo, huenda ndoa hiyo isifungwe mpaka mwishoni mwa mwaka kwa kuwa hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa Septemba mwaka huu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms