Thursday, March 1, 2012

........FILAMU YA PASTOR'S WIFE KUNITOA KIVINGINE........


MSANII wa filamu Esther Flavian, amesema kuwa anakamirisha kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Pastor’s Wife’, ambayo itakuwa sokoni wiki chache zijanzo.

Akizungumza, msanii huyo alisema kuwa huo ndiyo ujio wa mpya kwa mwaka huu na kilichobaki katkika filamu hiyo ni kumalizia kuhariri ili iweze kwenda sokoni.

Aliongeza kuwa filamu hiyo itakuwa inahusu maisha ya mchugaji na mke wake pindi wanapokuwa nyumbani hivyo ni stori ambayo inataeleza maisha halisi yanavyokuwa kwa watu hao
“Filamu imekamilika hivyo nawasihi mashabiki wangu wakae mkao wa kuipokea kwa sababu itakuwa na matukio mengo ya kusisimua ambayo hayana mfano hivyo kazi kwao,” alisema.

Pia msanii huyo alisema kuwa wanaomba mashabiki wao wote watakao itazama kazi hiyo watoe maoni yao ili kuweza kujua wapi wamekosea.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms