Monday, March 5, 2012

........CLOONEY HAKOSESHWI USINGIZI NA SHUTUMA ZA USHOGA........

AMEWAHI kuwa na uhusiano wa kimpenzi na mtangazaji wa televisheni wa Italia, Elisabetta Canalis na mwanamitindo wa Uingereza, Lisa Snowden, lakini tuhuma za ushoga zimekuwa zikimwandama mwigizaji, George Clooney.

Baada ya kuwepo kwa tetesi hizo kwa miaka mingi, staa huyo amelizungumzia jambo hilo akisema halimuumizi kichwa.

Siyo kwamba sisikii watu wakizungumzia habari hizo juu yangu, nimeamua kunyamaza kwa kuwa nina sababu nyingi za kufanya hivyo, alisema.

Kwanza nitakuwa sijitendei haki kuanza kujielezea undani wangu, lakini nikikataa nitakuwa nimewaumiza rafiki zangu wa karibu wanaojihusisha na vitendo hivyo, anasema Clooney.

Hivi sasa Clooney yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mcheza mieleka wa zamani wa WWE, Stacey Keibler.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms