Thursday, March 29, 2012

..........ALAH MILIONI 18 ZIMENITOKA KUKAMILISHA FILAMU HII...........

MTAYARISHAJI wa tamthili na filamu Tanzania, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuzi’, amesema, kuwa filamu yake ya ‘Tatakoa’, imetumia sh mil 18, na sasa ipo katika hatua za mwisho kutoka.

Mr Chuzi alisema kila kitu kimekamilika na kikubwa kinachoendelea sasa ni uhariri na baada ya hapo wataizindua ili mashabiki wao waweze kujua ni kitu gani kinachokwenda sokoni.

Alisema kuwa imetumia kiasi hicho cha pesa ni kutokana na malipo ya wasanii waliocheza, chakula, ulipaji wa maeneo walichezea, usafiri, wapiga picha na watu wengine wengi ambao wamehusika katika kuitengeneza kazi hiyo.

“Ni kiasi kidogo tofauti na filamu za wenzetu wa nje lakini tunashukuru kwamba tunafanya kile ambacho tumepanga hivyo naweza kusema kila msanii alicheza katika filamu ameonesha uwezo wake kwa lengo kusapoti kazi za Tanzania,” alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms