Wednesday, March 7, 2012

.........AKINA MA ATUNAWEZA TUKIWEZESHWA......

KATIKA kuadhimisha siku ya wanawake duniani ‘Women’s Day’, ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka, msanii Rose Ndauka, amesema kuwa anawashauri akina mama kuacha kuwa tengemezi badala yake wajikite katika kufanya kazi na kuleta maendeleo katika familia zao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na mwandishi wetu, msanii huyo alisema kuwa baadhi ya wanawake bado wanakasumba ya miaka 47 iliyopita kuwa wanaume ndiyo watu wanaoweza kuleta maendeleo ya taifa na familia kitu ambacho kwa upande anakipiga.

Alisema anaamini wapo wanawake wengi wanaotafuta maendeleo lakini baadhi yao wamekuwa wakikatishwa tamaa na wanaume wasiyo na uelewa wachache wasiyo na aibu.

“Siyo kwamba wanawake hatutaki kufanya mambo mazuri lakini baadhi yetu tumekuwa tukikata tamaa pale tunapotaka kufanya jambo fulani,” alisema.

Aliongeza kuwa anaamini siku hii maalumu kwa wanawake ambapo wengi wataelimika kwani kuna makongamano mengi ambayo yataeleza namna mwana mama anavyotakiwa kuishi ili aweze kuleta maendeleo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms