Monday, March 26, 2012

.......AFANDE SELE AMSHUKIA CHID BENZ........... ASEMA BADO NI BWANA MDOGO.......


Msanii Afande Sele aligeuka mbogo baada kumjibu msanii mwenzake Chid beenz kuwa hawezi kumteka na hana uwezo huo kwani Afande ameshakua mwanajeshi JWTZ na akaacha jeshi hivyo awezi kutishiwa amani na raia kama Chid Beenz.
"mimi nimekua kilipwa mshahara wa Jwtz na nimekulia hapo kariakoo iweje natishiwa na mtoto aliekulia Ilala" ALIONGEA AFANDE
Hii ilikuwa katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV ambapo Afande alifunguka mbaya kwa kitendo chaChid Benz kumwambia atamteka,hata hivyo afande alielezea jinsi anavyomfahamu Chid na anamchukulia kama bwana mdogo tu.
Pia aliweka wazi nia yake ya kutaka kugombea ubunge 2015 ,hivyo Chid ameombwa kumuomba radhi Afande kwani asipofanya hivyo ni kama anajimaliza kisanaa kwani ni wazi anatambua Afande ana mashabiki wengi na kwa kitendo alichokifanya Chid sio cha kiungwana.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms