Friday, February 17, 2012

........WALISEMA HATAOLEWA, MBONA KAOLEWA NA ATAFUNGA NDOA JULY......

NYOTA ndani ya bongo movie, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, sasa ameweka wazi kuwa ndoa yake na mfanyabiashara wa mafuta wa mkoani Tanga, itafungwa mapema mwezi Julai mwaka huu, kutokana na mchakato unaoendelea kufanyika.

Mtandao huu ulilipoti habari ya kuchumbiwa kwa msanii huyo mkoani Tanga, lakini sasa kila kitu kimewekwa wazi na atakuwa ndani ndoa mwezi Julai.

Akizungumzia ishu hiyo Shilole, alisema kuwa ameamua kuweka wazi ndoa yake kwani anapenda mashabiki wake waweze kujua nini kinachoendelea katika maisha yake.

“Nilikuwa sitaki watu waweze kujua kuhusu ndoa yangu, kwa sababu siyo tangazo lakini nimeona bora niweke wazi ili mashabiki wangu waweze kujua ishu hiyo ambayo itakuwa ya kihistoria sana,” alisema.

Hata hivyo msanii huyo hakutaka kumtaja jina mume wake mtarajiwa kwa kile alichodai kuwa ni mapema na anataka iwe zawadi kwa mashabiki wake.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms