Wednesday, February 29, 2012

........WALIOCHUKUA FOMU KUSHIRIKI BIG BROTHER NI ZAIDI YA WATANZANIA 500, WALIORUDISHA FOMU NI 100 TU.........

Muda wa kuchukua na kurudisha fomu tayari umekwisha feb 27, na idadi ya watanzania waliorudisha fomu mpaka sasa imetajwa kuwa ni 100 kwa Dar es salaam pekee.
Barbara Kambogi afisa uhusiano wa multichoice Tanzania amesema Kama bado hujajaza fomu na unataka kushiriki, usipate tabu siku za usaili unaweza kwenda hata kama hujajaza fomu na utaingia kwenye usaili kama kawaida, kama walivyoingia waliojaza fomu.
Shindano la big brother afrika mwaka huu linaanza may 6 ambapo ni lazima watu waende wawili wawili, unaweza ukaenda na mama yako, mpenzi wako, mume wako, mke wako, binamu, rafiki au yoyote mwingine.
Swali moja ambalo nilikua na kiu nalo, na nimepata jibu lake ni kuhusu watu waliorudisha fomu wamejaza kina nani watakaokwenda nao?
Watu wengi wamechagua kwenda na rafiki zao tu, wengine magirlfriends zao, wanaofata ni boyfriends, wengine wamechagua ndugu zao kama binamu ila wazazi kama mama sijaambiwa kabisaaa.
Kuna Dola laki tatu, jiulize ukishinda hizo pesa utafanya nini ? ni hela nyingi sana

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms