Friday, February 3, 2012

.........WA-MASAI NA DESTURI ZAO......... MWANAUME MMOJA , WAKE 20.......

Wajanja blog team, kwanza hongereni sana kwa kazi mnayoifanya. Aidha ningependa kuchukua fursa hii kuelezea kile nilichokiona na kukisikia wakati nilipokuwa kwenye mapumziko hapa nchini kwangu nikitokea Canada ninakofanyia kazi. 
Niliapa kuwa sitamaliza muda wangu wa mapumziko bila ya kufika bunga za wanyama za Ngorongoro, nilianza ziara yangu vyema na nikiwa katikati ya bunga ya wanyama ya Ngorongoro niliona BOMA moja kubwa la Kimasai. Nilivutiwa na Boma hili na ndipo nilipoamua kwenda kutembelea katika BOMA hilo, Nilikaribishwa vyema na wenyeji. 
Niliona watoto wengi sana kwenye boma hilo na ndipo nilipoamua kuuliza maswali mawili matatu hivi. Niliambiwa kuwa kwenye boma hilo kuna wanawake 20 na wote wako chini ya utawala wa mwanaume mmoja. Binafsi nilishangazwa sana na jinsi wamasai wanavyoweza kutunza amani kwenye familia kubwa kama  hii. Wengi waliniambia kuwa hii ni desturi ya wamasai wengi kwamba mwanaume anaoa wanawake zaidi ya mmoja.

Ni mimi Laurensia Denis

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms