Wednesday, February 29, 2012

.........TOYONI YUKO KWENYE HALI NGUMU..........

UHUSIANO wa kimapenzi uliokuwapo baina ya msanii Toyin Aimakhu na Kunle Soyombo umeyeyuka.

Wawili hao waliodumu kwa miaka kadhaa, walianza kutibuana Desemba mwaka jana, lakini Toyin akawa anafanya siri kwa watu wake wa karibu.

Toyin amekuwa akijaribu kutatua matatizo yake kimya kimya, lakini habari za ndani zinadai kuwa mwanaume huyo hataki kumwelewa ndiyo maana wamefarakana.

Familia za wawili hao zilishapewa utambulisho, lakini kasheshe ilikuja kwenye kufanya maamuzi ya mwisho ikiwemo harusi, jambo ambalo lilizua utata.

Marafiki wa karibu wa binti huyo, wanadai kuwa amekuwa akimpenda sana mpenzi huyo na imekuwa ngumu kumsahau kwani hata katika uso wa Blackberry yake ameweka picha ya Kunle na kuandika kwamba hakuna chochote anachoweza kukifananisha na mwanaume huyo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms