Friday, February 24, 2012

.....SONGEA MAMBO BADO SIYO SHWARI.......

Baada ya Polisi mkoani Ruvuma kuthibitisha kwamba watu wawili wamefariki dunia kwenye maandamano ya waendesha pikipiki juzi mjini Songea feb 22 2012, vurugu zameendelea tena jioni ya feb 23 ambapo ilibidi Polisi waongezwa kutoka nje ya mji ili kutoa usaidizi.
Mwandishi wa habari Innocent Harris amesema “kulikua na watu watatu walioshikwa na wananchi huko Lizabone mjini Ruvuma kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya hivi karibuni, mauaji ya kufululiza ambapo polsii katika harakati za kuwaokoa kuwapeleka polisi wananchi hao waliingilia kati na kutaka polisi wawaachie watu hao ili wawaadhibu wenyewe kitu ambacho kiliwafanya wananchi hao kusogea karibu na kitu cha polisi ambapo polisi walianza walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya ambapo wengi walianguka kutokana na mishtuko ya mabomu hayo”
Harris amesema pamoja na kwamba baadhi ya biashara zilizofungwa zimeanza kufunguliwa, bao hali sio shwari na magari ya polisi yameongezeka kutoka nje ya mji huo, na watu wanaishi kwa mashaka ambapo watu wageni katika mji huo wamepewa tahadhari ya kutotembea ovyo kwa sababu raia wa mji huo wanawashuku kwamba ndio wanahusika na mauaji ya kufululiza ya watu mbalimbali wasio na hatia, ambao wamekua wakiuwawa kikatili huku wengi wakiamini ni kwa sababu ya imani za kishirikina.
Bado millardayo.com inaendelea kumtafuta kamanda wa polisi Ruvuma, lakini tahadhari ni kwamba Wageni katika mji huo watakua na wakati mgumu kama wakikutana na wananchi wa eneo hilo alafu wakashindwa kujitambulisha vizuri.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms