Tuesday, February 28, 2012

......SKYNER KUTOKA KIVINGINE ZAIDI......

MSANII wa filamu bongo Skyner Ally ‘Skyner’, amefunguka na kudai kuwa baada ya kucheza filamu nyingi za kushirikishwa sasa anajiandaa kutoa filamu yake mwenyewe ambayo itakuwa na nyota kiao wa tasnia hiyi.

Akizungumza, mdada huyo alisema kuwa amecheza kazi nyingi hivyo hata kama atasisima mwenyewe anaamini kazi yake itafanya vizuri.

Aliongeza kuwa filamu yake hiyo kwa sasa bado hajaiopa jina kwani yupo katika mchakato wa kuangalia wasanii ambao wanaweza kucheza katika kiwango ambacho anahitaji ingawa wapo baadhi ya nyota ambao majina yao yapo kichwani.

“Unajua nimecheza sana filamu za watu hasa ‘Ray’, lakini kwa sasa nahitaji kuisisima mwenyewe na kuonesha uwezo wangu, ingawa naamini iyakuwa nzuri kwa sababu najipaga kuifanya iwe ni moja kati ya kazi zitakazofanya vizuri kimataifa,” alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms