Friday, February 10, 2012

......RITA NA INI EDO HAKUNAGA MAELEWANO BADO............

BADO hakuna amani baina ya mastaa wawili wa Nollywood, Rita Dominic na Ini Edo-Ehigwene, ambao wameingia mitini walipotaka kupatanishwa na marafiki zao wa karibu.

Wasanii hao wamekuwa na bifu la muda mrefu ingawa hakuna sababu ya msingi iliyoelezwa zaidi ya wivu wa kike baina yao, kibaya zaidi hakuna aliye tayari kushuka chini ya mwenziye.

Kila mmoja anajiona ni staa na ana uwezo zaidi na anaona wivu anapoona mwenzake akivuma kimataifa na kupata mikataba minono ya kibiashara.

Habari zinasema kuwa marafiki wa karibu wa wasanii hao pamoja na prodyuza mmoja maarufu, walitaka kuwapatanisha katika hoteli moja, lakini hakuna yoyote kati yao aliyetokea kwenye kikao hicho na kuwaacha wajumbe wakishangaa.

Ingawa jambo hilo linaelezwa kufanywa kwa siri, baadhi ya marafiki wa karibu walidaiwa kupenyeza umbea ndio maana mastaa hao wawili wakashtuka na kila mmoja kuingia mitini bila kutoa sababu za msingi. Kazi ipo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms