Thursday, February 2, 2012

....NYAMIDELA AJINADI KWEUPE........

MCHEKESHAJI wa kike anayefanyua vizuri Bongo, Sarafina Kindole Nyamidela ametamba kuwa ataongeza ubunifu zaidi mwaka huu ili kuthibitisha kwamba anastahili kuwa mwanamke pekee katika fani hiyo ya uchekeshaji.

Msanii huyo yupo katika kundi la Kash Kash ambalo uonyesha vichekesho vyake kupitia kipindi cha Mizengwe katika televisheni ya ITV.

Najua kuwa wasanii wa kike tupo wengi lakini ni katika filamu ambazo ni siriazi ila katika fani ya uchekeshaji nipo pekee yangu tu, angalau siku za nyuma walikuwepo akina Bi.

Kirobo na Matumaini lakini kwa sasa katika Televisheni nipo pekee yangu, kuchekesha ni kazi tofauti na kumliza mtu,anasema Nyamidela.

Msanii huyo anasema kuwa hali hiyo inatokana na wasanii hasa wa kike kushindwa kuwachekesha watazamaji nafasi ambayo imechukuliwa na wasanii wa kiume, anaamini kuwa kutengeneza filamu na mtu akalia ni rahisi lakini si kumchekesha mtazamaji, binti huyo ambaye pia ni MC anasema kuwa pamoja na kuwa pekee lakini kupitia fani hiyo ya uchekeshaji ameweza kuendelea kwa maana ya kipato tofauti alivyokuwa awali.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms