Tuesday, February 21, 2012

........NATAMANI UBUNGE.........

MSANII wenye vituko bongo movie, Baby Mahada, amesema kuwa malengo yake aliyojiwekea ni kuja kugombea ubunge anauwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, msanii huyo alisema kuwa hashindwi kuwatumikia wananchi hivyo baada ya miaka kadhaa atakuwa katika mchakato huo.

Alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya kutaka kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na vitendo vya baadhi wanasiasa kutowajali wananchi ambao ndiyo waliyowapa dhamana.

“Malengo yangu ni kuja kuwa mbunge na kikubwa ambacho nataka kukifanya ni kuwatumikia Watanzania, ambao kila siku wanalia juu ya wasansiasa ambao wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya maisha yao binafsi,” alisema.

Hata hivyo mwandisi alimuuliza swali, msanii huyo kwamba atatumia chama gani katika mchakato wake huo, ambapo alijibu kuwa hataki kuweka wazi chama chake lakini muda ukifika kila mtu anaweza kujua.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms