Tuesday, February 14, 2012

........MWANAUME WANGU HATOKI NJE.........HAKUNAGA DEMU MWINGINE WA KUMVUTIA ZAIDI YANGU.........

MSANII wa bongo movie Jackline Wolper, amefunguka na kusema kuwa hakuna mwanamke anayeweza kumchukua au kutoka na mpenzi wake pengine yeye ndiye anayeweza kuwachukua mabwana zao ingawa hana tabia hiyo chafu.

Wolper alisema kuwa mpenzi wake ni mtu ambaye anajiheshimu hivyo hana tabia chafu ambazo zinaweza kuharibu mapenzi yao kwani wanapendana na hakuna anaweza kuwatenganisha.

“Nasema hakuna msanii ambaye anaweza kutoka na mpenzi wangu, kwanza hana tabia za kihuni mapenzi ninayompa yanamfanya asiwe na mawazo ya kunisaliti hivyo natoa ukweli kwamba hakuna hata mmoja anayeweza kumchukua,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa mpenzi wake si mtu anayependa kujichangaya na wasanii wenye tabia za kuhuni kwani ni mtu ambaye yuko bize na kazi zake.

Wolper alisema siku zote mwanamke mrembo hatoki na mwanaume mshamba, kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii wengine ambao si warembo ambao hata wachumba zao si wale wanaoweza kusisima mbele za watu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms