Friday, February 17, 2012

.......MKATABA WA SIMU WAZIDI KUMPA ULAJI NAMELESS......

Usafiri anaosukuma Nameless

Mwimbaji Staa wa Afrika Mashariki Nameless amefunguka na kusema kwamba alilazimika kuupiga chini mkataba mmoja kati ya miwili ya kampuni mbili tofauti za simu za mkononi, zilizotaka kufanya nae kazi.
Nameless amesema alichoangalia kilikua ni pesa nyingi ndio maana aliupiga chini mkataba mwingine na kuingia kwenye mnono ambao umempa mafanikio ya kutosha, kifamilia zaidi, na kimaisha zaidi.
Mkataba huo mnono umezidi kumuweka Nameless juu kwenye list ya wasanii matajiri kenya, akiithibitishia kwamba sasa anaendesha gari aina ya BMW X5.
Mikataba ya mitandao ya simu imekua dili kubwa kwa baadhi ya wasanii wa kenya wanaobahatika kuipata, ambapo mfano mwingine mzuri ni wa JUA CALI, ambae alikiri miezi miwili iliyopita kwamba Mkataba wake na Safari com umemuwezesha kujenga nyumba ya gorofa moja, kununua gari aina ya Noah pamoja na kujenga studio ya kisasa kabisa ya kurekodi.
Miongoni mwa kazi ambazo huwa wanafanya kwenye mikataba hiyo ni kuzunguka sehemu mbalimbali za kenya kufanya Tour na kuwa balozi.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms