Wednesday, February 1, 2012

......MIMI SIJISIKII MBONA......

MSANII ambaye ni movie star bongo, Wema Sepetu, pamoja na madai ya watu kuwa anamajivuno, amekanusha kauli hizo na kusema wao wanaomzungumzia ndiyo wenye tabia hizo. Baadhi ya watu wanaonekana kuzungumzia tabia ya msanii huyu huku wengi wakidai anajisikia kutokana na umaarufu uliokuwa nao.

Msanii huyu alisema umaarufu alionao haimaanishi anamajivuno lakini kikubwa ambacho anaamini ni kwamba watu  wanaomzungumzia kuna kitu wanakihitaji kwake.

Alisema pamoja na kauli za watu za kutaka kumchafua haoni sababu ya kuwa jibu kwani matatizo aliyopata hivi karibuni yamemtosha na haitaji kuongeza mengine.
“Najua kuna watu ambao wanapenda kuzungumzia mambo yangu lakini nachoweza kusema ni kwamba sina tabia za majivuno na mara nyingi nacheka na watu,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa amekuwa akicheka na kila na mtu huku baadhi ya watu wengine wanamsihi kuacha tabia hiyo kwani yeye ni mtu maarufu ambaye anahitaji kukaa sehemu ambayo haina watu wengi kwa lengo kufanya kazi za sanaa.

“Naweza kusema kwamba nakuwa karibu sana na watu kitu ambacho hakiruhusiwi kwa staa yoyote, kwa sababu hata Ulaya unaweza kukaa miezi 7 hujamuona msanii yeyote akikatisha mtaani lakini huku kwetu hatuna kitu kama hicho,” aliongeza Wema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms