Wednesday, February 1, 2012

......LOL, ETI LULU NI BIKIRA????? AJITANGAZA HADHARANI KUWA YEYE NI KIBURUDISHO SAFI.......

MWIGIZAJI wa filamu Bongo mwenye umri mdogo lakini machachari katika matukio ya mastaa Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni alitoa kihoja kama si kichekesho pale alipojinadi kuwa yeye ni msichana asiyemjua mwanaume yaani akimananisha kuwa yeye ni Bikira na hajiusishi kabisa na wanaume.
Hata pale alipoulizwa kuhusu wanaume ambao iliwahi kuripotiwa kuwa ni wapenzi wake, mtu kama Ali Kiba alidai kuwa ni rafiki tu wa kawaida japo kuna wakati alidai kuwa hana marafiki wa aina yoyote.
“Unajua mara nyingi ni maneno tu ya magazeti ambayo hupenda kuniandika hivyo lakini mimi ni binti safi na sina mambo hayo ya wanaume bado mdogo mimi,”alisema Lulu.
Hata hivyo pamoja na kuongea hivyo lakini mavazi aliyokuwa amevaa yalipingana na kauli yake kuwa ni binti mwenye maadili mema, haya tena ukiyashangaa ya Mussa utayaona ya firauni.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms