Wednesday, February 22, 2012

...........LINAH KUKWEA PIPA MARCH........


Baada ya kuukubali mwaliko wa kwenda kuimba kwenye stage moja na Usher Raymond Marekani, alafu akaukubali tena mwaliko wa mama laura bush kwenda na kurudi marekani kwa mara ya pili, Mwimbaji Linah Sanga ameukubali mwaliko wa tatu wa kurudi tena marekani kwa ajili ya showz.
Time hii anapelekwa na mbunge wa viti maalum (Chadema) Leticia Nyerere ambae anafanya showz kwa ajili ya kutangaza utamaduni wa Afrika, mavazi yanayovaliwa na wasanii wa Afrika, jinsi wanavyopafom na mengine.
Akiwa msanii wa kwanza na pekee kwenye hiyo tour atakayozunguka majimbo karibu 15, Linah ambae atakaa Marekani kwa miezi minne amesema show zake mbili za kwanza atapiga Washington DC, ambapo atakua mwenyewe kwenye stage na kuimba kwa kutumia instrumental tu na atakua anaimba na nyimbo za wasanii wengine pia.
Baadhi ya majimbo atakayotembelea ni pamoja na LAS ANGELES, CARLIFONIA, MIAMI – FLORIDA na TEXAS.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms