Friday, February 17, 2012

..........LIBYA MAMBO SI SHWARI HATA KIDOGO......

Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International linasema visa vya mateso, mauaji na watu kuzuiliwa bila kufunguliwa mashataka vimekithiri nchini Libya ambapo ukiukaji huo unatekelezwa na makundi ya wapiganji waliojihami ambao walimng’oa Muammar Gaddafi madarakani.
Walioathirika zaidi ni watu wanaohofiwa kuwa wafuasi wa Gaddafi, waafrika weusi na wahamiaji walioko Libya ambapo Kufuatia visa hivyo, makundi ya watu waliolengwa sana na visa hivyo wameanza kuyahama makaazi yao.
Shirika hilo limesema serikali mpya ya Libya imeshindwa kuwachukulia hatua watu wanaotekeleza vitendo hivyo ambapo Ijumaa hii, sherehe zitafanyika kote nchini Libya kuadhimisha mwaka mmoja tangu mapinduzi yaanze ambayo yalitarajiwa kuleta mabadiliko.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms