Saturday, February 11, 2012

............KUTANA NA MOSES SWAI,MTOTO ALIYEONGOZA FORM FORM.........

Mwanafunzi ambae ameongoza katika matokeo ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka jana Moses Swai (16) amekiri kwamba hajawahi kushika nafasi chini ya namba mbili toka aanze shule, yani kuanzia primary mpaka form four.
Moses ambae amemaliza Feza Boyz Dar es salaam, amesema kazi anayotaka kuja kuifanya baadae ni Udaktari, huku akizidi kufunguka kwamba hakua anatarajia kama matokeo yake ya form four yangeweza kumfanya afikie mpaka kuitwa na ubalozi wa Uturuki – Tanzania, ambao umemzawadia MP3 Player.
Kutokana na kufaulu kwake, Moses pia ameamplfy kwamba mpaka sasa kiasi cha pesa alichowah kupata kwa ujumla, pesa ambazo amekua akipewa kama zawadi ni zaidi ya laki tisa ambapo kiasi kikubwa amekua akipewa na baba yake, ambae pia amekua akimnunulia games mbalimbali.
katika mtihani wake wa mwaka jana, Moses amesema “msimamizi wetu hakua mnoko sanaaa kama wengine lakini hiyo haimaanishi kwamba tuliigiliziana, hapana! sikumsaidia hata mtu mmoja kwenye huo mtihani na wala mimi sikusaidiwa chochote na mtu yoyote”

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms