Thursday, February 2, 2012

.........JACKLINE KUTOKA NA FILAMU YA 'MR NO BODY'.........MAANDALIZI YAKE KUGHARIMU MILIONI 16.........

MSANII mwenye staili ya kipekee ndani ya bongo movie, Jackline Wolper, amesema kuwa filamu yake ya ‘Mr No Body’, inatarajia kutumia shilingi milioni 16 hadi kukamilika kwake.

Akizungumza kuhusu bajeti ya filamu hiyo nyota huyo alisema kiasi hicho cha pesa kitatumika kuwalipa wasanii pamoja shughuli nyingine zote zitakahusiana na filamu hiyo.

Alisema fedha hizo ni pamoja na chakula, malipo ya wasanii, sehemu zote watakazopigia picha za filamu hiyo, usafiri, ulinzi na mambo mengine.

Pia alisema kuwa ndani ya filamu hiyo kuna wasanii wengi lakini nyota ambaye atasimama naye kama mhusika mkuu ni ‘Tino’, ambaye anauwezo mkubwa katika kuigiza.

“Filamu yangu ambayo natarajia kuitoa mwenyewe ni hiyo na baada ya hapo nitakuja na kazi nyingine kali ambazo zitafanya vizuri kimataifa, hivyo nawaomba mashabiki wangu waisubiri filamu hiyo kwani itakuwa na mafunzo ya kutosha,” alisema Wolper

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms