Tuesday, February 28, 2012

...........HII NDO SINGLE ILIYOMPA ULAJI MWASITI KWA MIAKA SITA......

Mwimbaji Mwasiti Almasi ambae huu ni mwaka wake wa tano toka ameanza kujulikana kwenye muziki akiwa na jumla ya single nane zinazojulikana, leo amekubali kufungua kitabu chake cha kumbukumbu na kutaja wimbo miongoni mwa nyimbo zake, iliyomfanya apate mialiko mingi ya showz kuliko single yake yoyote mpaka sasa.
Amesema “Millard hata nikifa kesho, kesho kutwa Nalivua Pendo kiukweli ni namba moja kwangu, ilinifanya nikakaa kimya muda mrefu sana na nikaendelea kupata hela, ina nipa showz mpaka kesho kutwa, japo Hao, sio kisa pombe, na Souljah nayo japo watanzania hawajaielewa sana ila zimechangia kunipa kipato”
Mwasiti amethibitisha pia kwamba single yake ya nalivua pendo, imempa asilimia 95 ya show zote alizowahi kufanya, ambapo ameitoa good news nyingine leo kwamba baada ya kuwa kimya kwa miezi zaidi ya saba, leo katoa single yake mpya inaitwa Kisima inayozungumzia mapenzi tu, amesimama kama mwanamke ambae amependa.
Ameamplfy kwamba “kisima ni sehemu ambayo mahaba hayaishi kama unavyojua kisimani ni sehemu ambayo mtu anachota maji, ndio hivyo hivyo kwa kisima hiki mahaba hayaishi”

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms