Monday, February 6, 2012

........HAKUNAGA URAFIKI TENA KATI YA KAJALA NA AUNT EZEKIELY.......

URAFIKI wa wasanii wawili wa tasnia ya filamu bongo, Kajala na Aunty Ezekiel, umeanza kuingia dosari, baada ya tetesi kwamba wamechukuliana bwana huku wakijua kuwa wao ni marafiki wa karibu.

Baadhi ya watu wa karibu na mastaa hao, walifunguka  na kusema kuwa dalili hizo mbaya zimejitokeza hivi karibuni ambapo nyota hao walionekana wakipigiana simu za kutukanana.

Kajala na Aunty hivi karibuni urafiki wao ulikuwa ni wa hali ya juu ambapo hata hivyo baadhi ya watu walitabiri kuwa hawawezi kufika mbali kwani wote ni wanawake ambao wanapenda kujirusha.

Mmoja wa wasanii ambae anafanya kazi na nyota hao, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa siku ambayo Kajala anatoroka na mpenzi wa rafiki yake walikuwa sehemu moja wanakunywa, baada ya wote kulewa ndiyo mchezo huo ulipofanyika.

Alisema baada ya kufanya kitendo hicho alimtaarifu Aunty, kuwa asiwe na wasiwasi kwani mpenzi wake ameondoka naye na hawezi kurudi eneo la tukio kwani wako mbali.

“Unajua hawa walikuwa ni marafiki sana na naweza kusema awali walikuwa kama ndugu lakini baada ya kuchukuliana wanaume basi hali imekuwa mbaya na kwa sasa hawapeani hata salamu.” alisema msanii huyo.
Baada ya warembo hao kutafutwa, Kajala, alisema kuwa hana bifu na Aunty lakini tatizo ambalo lipo ni dogo na watalimaliza kwani mapenzi hayana mwisho katika hii dunia.

Alisema alimchukua mpenzi wa rafiki yake lakini siku hiyo alikuwa amelewa na hakujua kama anafanya makosa makubwa kama hayo.

“Unajua pombe zikiwa zimepanda kichwani unaweza kufanya kitu ambacho hukutegemea kukifanya, lakini kuhusu hilo naweza kusema kwamba yataisha kwa sababu sisi marafiki wa kushibana,” alisema Kajala.

Kwa upande wa Aunty alidai kuwa hawezi kurudiana tena na mpenzi wake huyo ambaye tayari amelala na Kajala kwani haitaji kutoka na mwanaume ambaye tayari ametembea na msanii.

Aliongeza kwa kusema kuwa endapo Kajala, anahitaji waendelea kuwa marafiki basi amuombe msamaha kupitia vyombo vya habari ili kila mtu aweze kujua kilichotokea kati yao.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms