Tuesday, February 21, 2012

......CHRIS BROWN AWASHUKIA WANAOMKEJELI.......

USHINDI wa Tuzo ya Grammy alioupata wiki iliyopita umefanya jina la Chris Brown lipambe vyombo vya habari duniani kote, lakini wengi wakiupinga.

Hata mastaa kama Miranda Lambert na Jack Osbourne waliandika katika mtandao wa twitter kuelezea mshangao wao juu ya ushindi wa kijana huyo.

Kilichowafanya wengi wapinge ushindi huo siyo kuwa hajui kuimba, bali ni tukio alilofanya miaka miwili iliyopita la kumpiga na kumuumiza vibaya aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna huku tuzo zikiendelea kutolewa ukumbini.

Hata hivyo, Brown amewatolea maneno makali wote wanaopinga ushindi wake, huku akijitetea kuwa kila mtu anastahili kupewa nafasi ya pili anapokosea.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms