Thursday, January 19, 2012

.......UWEZO WAKO NI KILA KITU KATIKA FANI........

MCHEKESHAJI mahiri Bongo Athuman Mwalubadu King Mwalubadu anaamini kuwa msanii au mchekeshaji kuwa bora si lazima uigize katika filamu au komedi nyingi bali ni uwezo wako kwa kila kazi ambayo unashiriki na kuonyesha uwezo.

Maisha ya leo inakubidi uwe kama Sungura, bila ya hivyo unaweza kupotea katika fani, mimi sitaki kuamini kuwa kuigiza filamu nyingi au komedi nyingi ndio uwe bora lakini kama una uwezo katika kazi yoyoye, hata upewe nafasi kidogo tu watu watakuona kama umefanya kitu.

Baada ya kusoma soko niliona bora kuwa na kazi nyingine, hii inanisaidia katika kuchagua kazi za kufanya, anasema King Mwalubadu.

Msanii huyo ambaye aliwahi kuibuka Mchekeshaji Bora kwa mwaka 2010 kupitia tuzo za Wasanii Bora za 2010, amekuwa ni kivutio kwa wapenda komedi kwa staili yake ya kuigiza kama Mpemba.

King Mwalubadu ni mtangazaji katika kituo cha Redio cha Ibony Fm mkoani Iringa na ameshiriki katika komedi nyingi kama Inye, King Mwalubadu katika filamu ya Swahiba na Mahabuba

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms