Sunday, January 8, 2012

......USIACHE KUSOMA MESEJI HII KUTOKA KWA MDAU WETU .....


HONGERA ndugu yangu naona umeuona, wengi walitaka kuuona, lakini wameshindwa, ni suala la kushukuru sana kuuona mwaka mpya, 2012.

Na katika mwaka huu mzima, akilini mwako amini kuwa Raha ya maisha kwa wanandoa iko kwenye ndoa, nyumba ndogo ni upumbavu.

Ndugu yangu matatizo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku; mama yako uliyekaa tumboni mwake huwa kuna nyakati mnakorofishana, itakuwa mtu uliyekutana naye ukubwani? Ni suala la kuelewa na kutuliza akili katika kuendesha maisha yako ya kila siku.

Wenye hekima hutafakari kabla ya kutenda; dalili kwamba wewe ni mwanaume pumbavu ni kutelekeza familia na kwenda kwa mwanamke mwingine, eti kisa umegombana na mke.

Dalili za mwanaume pumbavu zaidi ni yule anayetelekeza mke na watoto, hataki kuwasomesha wala kuwasaidia watoto, kisa kagombana na mama wa watoto au labda ana mwanamke mwingine.

Kuna jamaa mmoja mpumbavu aligombana na mkewe nikamsikia anasema: Na huyo mtoto utajua namna ya kumtunza.

Ndugu yangu mbona unakuwa huna akili kiasi hiki, kosa la mtoto kutotunzwa ni lipi? Tafakari ndugu yangu, hata mbwa huzipenda familia zao, mbona wewe unakuwa na tabia mbaya zaidi ya mbwa

Wewe ungekuwa mtoto ungejihisi raha kutelekezwa na baba yako? Ungejihisi raha kutelekezwa na mama yako? Ungejihisi raha kutolipiwa ada eti kisa baba na mama yako wamenyimana unyumba! Ndugu yangu vipi, hekima umeipeleka wapi

Kuna wanaume na akili zao, wametoa talaka kwa wake zao walioanza nao maisha na kutafuta wengine. Ndugu yangu siyo baraka kufukuza mke, eti labda kwa sababu siku hizi mambo yako yamekuwa safi kwa hiyo unaona kama vile yule wa mwanzo hana hadhi.

Mke au mume wa ndoa ya kwanza ni bora zaidi; Unaweza kukataa lakini ni vizuri zaidi kuvishikilia vitu tulivyoanza navyo toka awali. Kama inashindikana, basi kuwe na sababu za msingi. Wengi wana sababu za kihuni za kuachana.

Kuachana ni fikra potofu; ukiwa na shida kwenye ndoa, tafuta sababu ni nini? Kuna wengine utasikia Aah bwana ametoka nje kufanya na ngono na watu wengine, sitaki tena.

Ni sawa kwani hata vitabu vitakatifu vimeeleza kukerwa na uzinzi, mbona wengi wanaoa au kuolewa tayari wameshafanya ngono na wanaume au wanawake kibao, kwa uchache wawili, wengine hadi kumi.

Anaingia kwenye ndoa kachoka hoi! Sisemi kwamba kufanya uzinzi kuruhusiwe, lakini katika maisha hakuna kosa kubwa wala dogo, cha msingi ni namna tunavyoyachukulia makosa tunayotendewa.

Ni nzuri zaidi katika maisha kuwa na roho ya kusamehe. Utaacha wangapi ndugu yangu? Ni baraka zaidi katika maisha kuwa na roho ya kusamehe na kusahau.

Lakini ni upumbavu kwa wanandoa kulala vitanda tofauti au kulala vyumba tofauti hasa kama suala hili linafanywa kwa sababu mmoja amekasirika.

Ni vizuri kuwa na majadiliano kumaliza tofauti, badala ya kuendeleza migogoro.

Ndugu yangu, naona maneno ya kukumbushana yamekuwa mengi zaidi, kiasi kwamba huenda sasa ukashangaa mbona nasoma tu sioni sehemu inayofanana na kichwa cha habari kilichopo juu yaani Ukipewa ofa, subiri kuilipa, hakuna cha bure duniani.

Juzi nilikuwa napita eneo fulani nikakutana na kisa, waooo!! Kisa chenyewe ni hiki kwamba kuna binti eti kapewa ofa na mbaba, mjibaba Ofa ya kwenda bichi Bagamoyo.
Baba wa watu akakubaliwa ombi lake la kumpeleka kwenye ofa, watu hawa ni majirani tu.

Makubaliano ni kwamba wangekwenda huko asubuhi kwa kutumia gari la jamaa na wangelala hoteli ya kifahari ambayo huenda binti hakuwahi kulala tangu ametoka tumboni mwa mama yake.

Lakini baada ya mwanamke kuhoji staili ya kulala huko, akaambiwa kila mtu atakuwa na chumba chake! Aah utani huo! ha! ha! ha!

Lakini ambacho nataka kuwauliza wanawake ni kwamba sielewi kama ni kweli huwa hawajui au la.

Utawakuta wanawake wengine wanatumiwa ujumbe na wanaume ambao hawana uhusiano nao, umeamkaje Umekula Umelalaje? Ok niambie unasema umelala, umevaa nguo gani? Ooh ina rangi gani? Niambie nguo nyingine uliyovaa
Inatia kinyaa zaidi kuona anayeulizwa maswali haya naye anajibu. Kitaalam, kujibu nimevaa hivi, ni dalili kwamba unaelekea kuingia laini, kwanini unajirahisi

Ni mimi mdau mkubwa wa WB

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms