Tuesday, January 24, 2012

.......SIJAFULIA, BALI NILIUZA NYUMBA KWA MALENGO - MATONYA......

MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo, Matonya, amesema aliamua kuuza nyumba yake iliyopo mkoani Tanga, ili ajenge mjengo mpya, na si kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu kuwa amefulia.

Mwaka jana msanii huyo alidaiwa kuuza nyumba yake kwa madai kuwa amefulia na hana sehemu nyingine ya kupata pesa baada ya muziki wake kuwa mgumu sokoni.

Matonya alifunguka zaidi kuwa baada ya kuuza nyumba hiyo aliamua kujenga nyingine ambapo ujenzi wake unatarajia kumalizika June mwaka juu.

“Daa!! nashindwa hata kuelewa ni nani ambaye alijua nimeuza nyumba, lakini hata hivyo kila kitu kinaenda sawa kwani nimeuza na pesa zote nimezitumia katika mjengo wangu mpya ambao utakuwa ni zaidi ya niliyouza,” alisema

1 comments:

priss said...

hayatuhusu hiyo nijuu yako. ila umepotea sana kwenye gem.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms