Wednesday, January 11, 2012

......SASA MILUPO BASI ......NIMEVUTA WANGU NDANI.........

 Mchekeshaji mahiri Bongo, Mkwele Orijino, alifunga ndoa Ijumaa mchana katika mitaa ya Mabibo na Bi Fatma Abdallah Massawa na kusindikizwa na washirika wake wa karibu.
Kiongozi wa kundi lake la Kashikashi, Sumaku alisema; Kijana amekua, naweza kusema kwa maana nyingine, kuoa kwa vijana wa siku hizi si jambo la mchezo, maana wanapenda sana mambo ya kujaribu jaribu.
Kijana wangu yupo safi, si kama wengine ambao kila siku wanasubiri maisha yawe mazuri ili waoe, sasa maisha yakiharibika inakuwaje, utaendelea kuzini Mke ana raha yake bwana usiangalie karaha, anasema Sumaku.
Sherehe zilifanyika katika ukumbi wa Deluxe Hotel Sinza Kijiweni, huku mpambe wake akiwa pia ni mchekeshaji mwenzake Maringo Saba sambamba na Mzee Matata.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms